Katika mitandao ya kijamii kama vile Facebook,instagram na Twitter kumekua na gumzo juu ya yale mambo ambayo mtu asiefahamika amekua akiyasema na kuyaweka mtandaoni kuihusu Serikali.WaTanzania wengi wamekua wakijiuliza ni nani huyu na anatoa wapi mambo ambayo huenda yakawa nyeti sana kwa serikali ya Tanzania.
Hii imesababisha kutokea kwa mgawanyiko kati ya Watanzania,wengine wakimuunga mkono na wengine wakilaani kwa yale anayoyazungumza.swali ni je,huyu mtu ni Mwanaharakati kwa uhalisia wake au ni kibaraka wa mabepari?
KIGOGO 🇰🇪 kama anavyojiita kwenye mitandao ya kijamii amejielezea yeye mwenyewe kua yeye ni nani na ana lengo gani kwa taifa lake.
Katika ukurasa wake wa Twitter KIGOGO 🇰🇪 amejielezea yeye kua ni "Mwanaharakati wa kudumu wa haki za binadamu na uhuru wa kusema na mwanzilishi wa FichuaTanzania.org na fichua Technology LLC .."
Jambo la kustahajabisha ni kwamba huyu mtu hana nia ya kuacha yale ambayo anadai kuyatenda kwa faida ya Tanzania.Anamalizia kwenye ukurasa wake wa Twitter kwa kusema "KEEP ATTACKING 🔥✌️"
Hebu tuangalie yale anayodai kua ni ukombozi na uhalisia wa mzalendo kwa nchi yake.Katika kujielezea kwake anamalizia na alama ya ✌️ ambayo wote tunajua kabisa kua ni alam ya Chama Cha Demokrasia na Maendeleo(CHADEMA).Swali ni je,huyu ni mfuasi wa Chadema?...nadhani unaweza kujiuliza hilo swali kisha ujijibu.
Mwanaharakati huyu,kama anavyodai,amekua akipamba moto zaidi katika kipindi cha uchaguzi ambapo amekua akitoa matokeo ya uchaguzi kabla hayajatoka na watu wamekua wanajiuliza "amewezaje kuyajua haya?",na pia aliweza kutoa taarifa juu ya mambo mbalimbali yanayoendelea nchini kwa madai ya kua serikali inaua watu wake.
Swali la changamoto kwa mpenzi msomaji wa makala hii:Je,ukimuona mama yako anatoka nje ya ndoa,utaenda kutoa taarifa kwa Baba au utaongea na mama kwa siri na kumkana juu ya uovu wake?
Labda nikufungue macho Mtanzania mwenzangu,kuwagombanisha mama na baba kwa sababu ya ukahaba wa mama sio kutatua tatizo bali ni kuongeza tatizo juu ya tatizo.Na madhara zaidi yanaweza tokea kama vile baba kumuua mama kwa hasira au mambo mengine yanayoendana na hilo kwa kiwango chake.
MAONI YA MWANDISHI:TANZANIA 🇹🇿 NI MIMI NA WEWE!
Mmoja wa watu mashuhuri alishawahi sema kua "Taifa ni watu lakini sio sehemu".
Huenda ikawa ni kweli serikali inamakosa inayafanya lakini KIGOGO 🇰🇪 anatumia hayo kwa lengo la kuisambaratisha nchi.Vita vya wenyewe kwa wenyewe ni vibaya mno,twaweza chukua mfano toka kwa Rwanda na mauaji ya kimambali.
Kama mimi na wewe hatutolitetea taifa letu dhidi ya wale wanaotaka kututenganisha basi mwisho wa siku tutaaangalia Tanzania ikigeuka kua majivu na huku tukipoteza wapenzi wetu na malengo yetu kuyeyuka.Ndipo tutakapokua mfano kwa mataifa mengine huku watu kama KIGOGO 🇰🇪 wakiwa mbali na kusheherekea utimivu wa lengo lake pamoja na wale wanaompa nguvu ya kuwatawanya Watanzania
Unakaribishwa msomaji kwa kutoa maoni yako na mtazamo wako juu ya hili swala,Karibu!
.
0 Comments