Siku chache baada ya video ya Rayvanny na Paula kuvuja mtandaoni,Kajala mama mzazi wa Paula alisimama na kudai kua aliesababisha hayo yote ni Hamissa Mobeto,mzazi mwenza wa Diamond Platnumz.

Kajala,alidai kua Binti yake alitoka "out" na Hamissa ambapo masaa 12 baadae ndipo video ilipoachiliwa mtandaoni hali iliyomfanya Kajala kulaani kitendo hicho huku Harmonize akimuunga mkono.

Jambo jipya la hivi punde ni kwamba, Hamissa amemfungulia mashtaka Kajala kwa madai kua amemchafulia heshima yake na hivyo kupewa masaa 12 aombe radhi na kufuta post yake kwenye mitandao ya kijamii.

Soma barua hizo hapa: